Published on Africa Can End Poverty

Africa Development Forum: Utafiti Mpya na Mitazamo kutoka kwa Ushirikiano Wetu wa Miaka 15 kwa Ajili ya Maarifa

This page in:
Africa Development Forum: Utafiti Mpya na Mitazamo kutoka kwa Ushirikiano Wetu wa Miaka 15 kwa Ajili ya Maarifa

This page in: English | Français | Kiswahili


Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, mtazamo kuhusu maendeleo ya Afrika umebadilika kutoka dhana ya Africa Rising hadi hali halisi yenye changamoto nyingi tunazoshuhudia leo. Ingawa kumekuwepo na ukuaji wa uchumi, na tunatarajia Afrika itaendelea kukua kwa wastani wa asilimia 4 katika miaka mitatu ijayo — ikiwa nafasi ya pili baada ya Asia Mashariki na Kusini — ukuaji huu haujapelekea ustawi mpana kwa watu na jamii. Umaskini wa kupindukia bado ni tatizo sugu, na Afrika bado ni bara la pili lenye pengo kubwa zaidi la usawa duniani. Kanda hii inaendelea kupata ongezeko kubwa la watu, lakini nafasi za ajira hazitoshelezi kuyakidhi mahitaji hayo. Ifikapo mwaka 2030, vijana wa Kiafrika wapatao milioni 170 watakuwa wakihitaji elimu — na mamilioni zaidi watahitaji kazi zenye staha. Kwa maneno mengine, Afrika ni bara lenye fursa kubwa lakini pia changamoto ngumu.

Kuwawezesha watunga sera na watoa maamuzi kwa mageuzi yanayozingatia ushahidi ni jambo la msingi katika kuamua mustakabali wa Afrika — na huu ndio msingi wa mfululizo wa Africa Development Forum, ushirikiano wa maarifa ulioanzishwa mwaka 2010 na Ofisi ya Mchumi Mkuu wa Afrika ya Benki ya Dunia pamoja na Agence Française de Développement (AFD), ukiratibiwa na Kitengo cha Uchapishaji cha Benki ya Dunia. Kwa machapisho 37 hadi sasa na idadi ikiwa inaendelea kuongezeka, mfululizo huu umeunganisha watafiti mashuhuri, takwimu muhimu, na maarifa ya vitendo ili kujibu hoja za muda mrefu kuhusu maendeleo ya Afrika — ikiwemo miundombinu, biashara, nishati, elimu, na kilimo. Kwa miaka mingi, mfululizo huu umeendelea kukua huku ukidumisha viwango vya juu vya ubora, na wakati huo huo ukifungua milango kwa waandishi na taasisi zaidi za utafiti kutoka barani Afrika. Hivi karibuni, Benki ya Dunia na AFD pia zimeamua kutafsiri machapisho zaidi kwa lugha za Kiafrika ili kuwafikia wasomaji wengi zaidi.

Mwaka huu unaadhimisha miaka 15 ya Africa Development Forum. Ili kusherehekea hatua hii muhimu, Benki ya Dunia na AFD wanazindua mfululizo wa blogu zitakazoandikwa na wataalamu mashuhuri ambao wataangazia upya mada kuu za Africa Development Forum kwa kutumia takwimu mpya na mitazamo ya sasa.

Tunaanza mwezi ujao na blogu kutoka kwa Justice Mensah, itakayochambua changamoto ya kupanua upatikanaji wa umeme na miundombinu katika bara zima.

Tunatarajia kwamba uchambuzi wake — pamoja na wa wengine katika miezi ijayo — utatoa mitazamo mipya kuhusu sera zinazohitajika kusaidia Afrika kushinda changamoto zake za maendeleo, kuunda ajira zenye staha, na kuendeleza ukuaji jumuishi kwa muongo ujao na zaidi. Hii ni sehemu ya dhamira ya pamoja ya Benki ya Dunia na AFD.

 

Related:  The AFD–World Bank Group Partnership: Powering Development Impact Through Collaboration


Join the Conversation

The content of this field is kept private and will not be shown publicly
Remaining characters: 1000